Header Ads

ad

Breaking News

ECOBANK Tanzania imezindua huduma za kibenki nje ya tawi

ECOBANK Tanzania imezindua huduma za kibenki nje ya tawi ambayo itarahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kupitia simu na mitandao ya kompyuta.
 
Mkurugenzi Mtendaji, wa wateja binansi na wajasiliamali wa Ecobank Africa, Patrick Akinwuntan (katikati) akiwa pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo wakielekea kwenye warsha iliyofanyika Hoteli ya Serena Dar es Salaam.
 
Mkurugenzi wa Ecobank Tanzania, Enoch Osei-Safo, alisema ushirikishwaji wa fedha utawapa Watanzania urahisi wa kupata huduma za kibenki hasa kwa watu ambao hawana huduma hizo.

Alisema uzinduzi huo ni dhana ambayo inaendelezwa ndani ya Ecobank Afrika na kwa Tanzania itarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa watu wa kipato cha chini ili kuendeleza uchumi wa nchi.

Osei-Safo alisema Ecobank Tanzania Limited ambayo ni moja ya makundi la Ecobank Afrika iko katika nchi 33 Afrika na inashirikiana na Kundi la Ushauri wa Kusaidia Maskini (CGAP) shirika la kimataifa la makazi katika benki ya dunia ili kuleta huduma za benki karibu na watu.

 
Mkurugenzi Mtendaji, wa wateja binansi na wajasiliamali wa Ecobank Africa, Patrick Akinwuntan (katikati) akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam Januari 31, alipoongea nao kuhusu upatikanaji wa huduma za kibenki bila kufika matawini nchini Tanzania Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo nchini, Enoch Osei-Safo na Mkuu wa Wateja wa binafsi na Wajasiriamali wa benki hiyo, Joyce Malei. (Picha na Mpiga picha Wetu)


Naye meneja wa teknolojia na uvumbuzi wa biashara, Steve Rasmussen (CGAP), alionyesha furaha kwa ushirikiano wa pamoja na Ecobank. Alisisitiza kuwa ushirikiano utajenga uwezo na kuandaa taasisi ya kuleta huduma za benki karibu na wananchi.

Pia Mkurugenzi Mtendaji, Wateja, Biashara na Wajasiriamali, Patrick Akinwuntan, alisema Ecobank itaendelea na jitihada za kukuza njia mbadala kama sehemu ya mkakati wa kuleta huduma za benki kwa wananchi.

No comments