Header Ads

ad

Breaking News

POLISI WAUNDA TUME MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI

Askari Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakimsulubu mtu anayedaiwa kuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten Iringa, Daud Mwangosi katika vurugu zilizotokea kati ya Polisi na wafuasi wa Chadema kwenye Kijiji cha Nyololo, Mufindi. Katika vurugu hizo mwandishi huyo aliuawa kwa kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu.
 Polisi wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakimsaidia mmoja wa askari aliyeruhiwa katika tukio la kuuawa kwa mwandishi Daud Mwangosi huko Nyololo, Mufindi mkoani Iringa
 Mwili wa Daud Mwangosi baada ya kusambaratishwa na bomu. Aliyekaa jirani ni askari ambaye alijeruhiwa katika tukio hilo
 Polisi wa FFU wakipiga mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ofisi za tawi la chama chao
 Mkuu wa Operesheni Sangara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Benson Kigaila, akiwa katika gari la chama hicho pamoja na mmoja wa majeruhi wa vurugu za polisi na wafuasi wa chama hicho
 RPC katika maandalizi
Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakipandishwa katika gari la Polisi


DAR ES SALAAM, Tanzania

JESHI la Polisi nchini limeunda tume itakayochunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten, Marehemu Daud Mwangosi kilichotokea mjini Iringa wakati Jeshi la Polisi likipambana na wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ufunguzi wa tawi la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja (pichani) amesema kuwa Uchunguzi huo utavishirikisha vyombo vya usalama kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) "Jeshi la Polisi limeunda tume itakayowahusisha Maofisa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ pamoja Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Robert Manumba, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu kiliochosababisha kifo cha mwandishi huyo basi tusubiri matokeo ya uchunguzi huo" alisema Chagonja.

Marehemu Mwangosi amefariki dunia jana wakati baada ya kulipukiwa na kitu kinachachodaiwa kuwa ni bomu wakati chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) kikifungua tawi la chama vchake katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

"Kwa sasa tayari Ispekta Generali wa Polisi (IGP), Said Mwema yupo mjini Iringa pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba pamoja na timu yake nzima kuanza rasmi kwa uchunguzi wa tukio hilo. Alisema Kamishna Chagonja".

No comments