KLABU KUTETEA PINGAMIZI ZA WACHEZAJI
![]() |
Alex Mgongolwa |
Klabu
zote zilizowekewa pingamizi za wachezaji kwenye usajili na zile
zilizoweka pingamizi zinatakiwa kufika kwenye kikao cha Kamati ya
Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kitakachofanyika leo.
Kikao hicho kitafanyika kwenye ofisi za TFF kuanzia saa 6 kamili mchana, na kitakuwa chini ya uenyekiti wa Alex Mgongolwa.
Klabu ambazo zimewekewa/ kuweka
pingamizi na zitakiwa kuwepo kwenye kikao zilikiwa na nyaraka zote
kuthibitisha madai yao ni Azam, African Lyon, Flamingo, JKT Ruvu, Kagera
Sugar, Oljoro JKT, Polisi Mara, Rollingstone Multipurpose Ateclass
Foundation, Simba, Super Falcon, Toto Africans, Villa Squad na Yanga.
No comments