MSAMA PROMOTION YASAIDIA MATIBABU YA MCHEZAJI WA ZAMANI WA TAIFA STARS
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama (kushoto) akimkabidhi msaada wa fedha taslimu sh. milioni moja mchezaji
wa zamani wa Simba, Mtibwa na Taifa Stars, Alphonce Modest kwa ajili ya
kumsaidia katika matibabu ya ugonjwa wa mifupa unaosababisha miguu kufa
ganzi ‘yabisi baridi’. Modest nasumbuliwa na ugonjwa huo tangu mwaka
2011. Kwa yeyote anayeguswa na tatizo lake awasiliane na mtangazaji wa
Chanel 10, Said Kilumanga (wa pili kulia) kwa kupitia namba 0718 427426.
Wa Pili kushoto ni Mhariri Kiongozi wa Champion, Saleh Ally.
Mtangazaji
wa Chanel 10, Said Kilumanga akizungumza na waandishi wa habari wakati
akitoa rai kwa watu mbalimbali kujitolkeza katika kumsaidia mchezaji wa
zamani wa Simba na timu ya Taifa Alfonce Modest ambaye anasumbuliwa na
matatizo ya miguu.
Beki
wa zamani wa Simba na timu ya Taifa, Alfonce Modest akimshukuru
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions baada ya kumsaidia kiasi cha
sh milioni moja kwa ajili ya kuanza matibabu ya miguu.
Mhariri
Kiongozi wa Champion, Saleh Ally akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu watu mbalimbali kujitokeza katika kusaidia matibabu ya mchezaji
wa zamani wa timu ya Simba na Taifa Stars, Alfonce Modest.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, ametoa msaada wa sh milioni moja kwa nyota wa zamani wa soka, Alfonce Modest.
Modest
aliyewahi kuwika na timu za Pamba ya Mwanza, Simba, Mlandege na Taifa
Stars, anasumbuliwa na matatizo ya miguu kukosa nguvu.
Akizungumza
wakati wa kutoa msaada wake kwa Modest kwenye Ofisi za Kituo cha
Televisheni ya Channel Ten, Msama alisema amefanya hivyo kutokana na
kuguswa na tatizo hilo.
Alisema, akiwa mdau wa masuala ya kijamii, ameona atoe hicho kidogo kama mwanzo wa fedha za matibabu kwa mkongwe huyo.
“Mimi nimejitolea kumsaidia ndugu yangu Modest, nimemsaidia kama Mtanzania mwenzangu, aliyewahi kutoa mchango mkubwa katika soka ya nchi hii,” alisema Msama.
Msama ambaye ni mwasisi wa matamasha ya muziki wa Injili nchini, amewataka wengine wenye moyo kujitokeza kumsaidia Modest.
Akizungumza
baada ya kupokea kiasi cha awali cha sh 600,000, alimshukuru Msama kwa
moyo wa kusaidia wenye shida na matatizo mbalimbali kwenye jamii.
“Nimekuwa nikimsikia tu Msama, kumbe ndiyo huyu, namshukuru sana, naamini sasa nitapata matibabu ya uhakika,” alisema Modest.
Aidha, alitoa shukrani kwa wote waliofanikisha suala hilo akiwamo Said Kilumanga na Saleh Ally.
Akizungumza
baada ya Modest kukabidhiwa msaada huo, Kilumanga alisema Modest
ataanza kupatiwa vipimo kesho kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kitengo la mifupa.
Alitoa wito kwa atakayeguswa na tatizo la Modest afike ofisi za Channel Ten kwa ajili ya kukutanishwa na mhusika.
Akielezea
kwa undani kuhusu tatizo lake, Modest alisema, matatizo ya afya yake
yalianza mwaka 2010, wakati huo alikuwa akisumbuliwa na mapafu kujaa
maji.
Alisema,
baada ya kulazwa kwa miezi mitatu katika Hospitali ya Lugalo, alipata
nafuu kiasi, lakini mwaka uliofuata 2011, akaanza kuhisi viungo kukosa
nguvu.
Alisema, licha ya kuhangaika huku na huko, tatizo hilo la ganzi kwenye viungo likazidi na kusababisha mwili wake kushindwa kuwasiliana.
“Ganzi
ilianzia kwenye viungo vya miguu, lakini sasa imepanda hadi kwenye
mikono na maeneo mengine ya mwili, kwa kweli naumwa, niombeeni kwa
Mungu, niweze kupona,” alisema Alfonce aliyestaafu soka mwaka 2002,
akiwa katika kikosi Mtibwa Sugar. www.francisdande.blogspot.com
No comments