Maximo apewa jukumu Yanga
![]() |
Maximo |
KOCHA wa zamani wa timu ya Taifa
‘Taifa Stars, Mblazil Marcio Maximo, amepewa jukumu zito la kuwatafuta
wachezaji wawili ili aje nao.
Maximo anatarajiwa kukinoa
kikosi cha Yanga msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, lakini kama tajiri wa klabu hiyo,
Yusuf Manji, ataukwaa uenyekiti.
Manji alichukua fomu za
kuwania uenyeji wa klabu hoyo, katika uchaguzi utakaofanyika Julai 15, mwaka
huu jijini Dar es Salaam.
“Manji ana mipango mizuri ikiwa atashinda,
kwanza anataka kumleta Maximo na kuwasajili wachezaji wawili kutoka Brazil,”
alisema.
Tajiri huyo katika nafasi ya
uenyekiti atakuwa akichuana na John
Jambele, Edger Chibura na Sarah Ramadhani.
Nafasi Makamu Mwenyekiti inawania
na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Ally Mayay, Ayoub Nyenzi, Yona Kevela na
Clement Sanga.
Waanaowania ujumbe wa kamati
ya utendaji ni Lameck
Nyambaya, Ramadhani Mzimba ‘Kampira’, Mohamed Mbaraka, Ramadhani Said, Edgar
Fongo, Beda Simba, Ahmad Gao, Mussa Katabaro, George Manyama na Aaron Nyanda.
Wengine
ni Abdallah Bin Kleb, Omary Ndula, Shaaban Katwila, Jumanne Mohamed Mwammenywa,
Abdallah Mbaraka, Peter Haule, Justin Baruti na Abdallah Sharia.
No comments