GAMBIA KUWASILI LEO USIKU
Wambura, Msemaji TFF |
Timu
ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) ambayo awali ilikuwa iwasili nchini
leo (Juni 7 mwaka huu) saa 1.40 asubuhi sasa itawasili leo saa 9.20
usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya
Taifa Stars.
The
Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini
kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya
ambapo ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.
Kikosi
cha timu hiyo chenye wachezaji 22 wakiwemo tisa wanaocheza mpira wa
kulipwa nje ya nchi hiyo kitafikia kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa
wa Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo.
Wachezaji walioko katika msafara huo ni Musa
Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman
Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay na
Demba Savage.
No comments