Martin Sospeter aeleza masikitiko yake
Meneja mpya wa bendi ya Mashujaa Martin Sospeter akizungumza na
waandishi wa habari wakati alipotangaza kujiunga na bendi hiyo kwenye
ukumbi wa Busness Kijitonyama asubuhi hii, kulia katika picha ni King
Dodoo Kaimu Meneja wa bendi ya Mashujaa.
Martin Sospeter katikati akilalamikia shutuma zilizoelekezwa
kwake na bendi ya African Stars wakati alipoongea na wanahabari asubuhi
hii kwenye ukumbi wa Busness Kijitonyama, kulia ni Kaimu Meneja wa bendi
hiyo King Dodoo na kushoto ni Rais wa Bendi ya Mashujaa Charles Baba.
Juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa
Asha Baraka katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa amenifukuza kazi kutokana
kuhujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa
Kwa kweli kauli ile ilinisikitisha sana
kutokana na ukweli kwamba, Asha nilimchukulia kama
zaidi ya dada kwani nilifanya naye kazi kwa
miaka 14, iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo
vya habari?
Mimi sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga
kuhamia Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya mwisho wa siku
kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutanghazwa kuhamia
Mashujaa.
Leo napenda nitangaze rasmi kwamba, nimeachana na African
Stars na kujunga na Mashujaa Entertainment na tayari nimeshasaini mktaba wa
kazi katika bendi hii.
“Nilipanga nifanye taratibu za kumuaga kutokana na kuwa,
nilikuwa nafanya kazi kwake bila ya mkataba, lakini nimepata bendi hii ambayo
tulikaa na kukubaliana mambo mbalimbali.
Mbali na mkataba, baadhi ya makubaliano na uongozi wa Mashujaa ni pamoja na kunipangia nyumba hali itakayonilazimu kuhama ile iliyokuwa
chini ya Twanga.
Ninaamini nitafanya vema kazi yangu hii mpya kama ilivyokuwa Twanga, ambapo nilidumu kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo nilipoachia, hivyo naomba ushirikiano kwa uongozi,
wanamuziki, Wadau na hata ninyi mwaandishi wa habari.
No comments