WAZIRI MAVUNDE AZINDUA KITUO CHA POLISI NGWALA-SONGWE.
Waziri wa Madini Anthiony Mavunde akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngwala mkoani Songwe wakati wa uzinduzi wa kituo kipya cha polisi katika kata hiyo Juni 4,2025
WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde, juzi Jumatano Juni 4,2025 amezindua kituo cha Polisi Ngwala mkoani Songwe chenye hadhi ya daraja la C kitakachotoa huduma kwa wananchi wa kata hiyo na maeneo ya jirani.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga ameishukuru kampuni hiyo kwa kujenga kituo hicho pia amewasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (lGP) Camilus Wambura kwa kumpongeza Waziri wa Madini kwa kuzindua kituo hicho.
Na Mwandishi Wetu, Songwe
Kituo hicho kimejengwa na Kampuni ya Madini ya Mamba kilichopo kata ya Ngwala Wilaya ya Songwe na Mkoa wa Songwe.
Akizindua kituo hicho Juni 4, 2025, Waziri Mavunde ameeleza dhumuni ya kujenga kituo hicho ni kwa kuwa kutakuwa na muingiliano wa watu ikiwa ni pamoja na mzunguko wa fedha kuwa mkubwa katika eneo hilo.

Amesema kutokana na mradi wa uchimbaji wa madini adimu duniani uhalifu utakuwepo katika eneo hilo hivyo, kituo hicho kitasaidia kupunguza uhalifu ili shughuli za kiuchumi ziendelee kwa amani na kuweza kuwanufaisha wananchi wa kata hiyo.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga ameishukuru kampuni hiyo kwa kujenga kituo hicho pia amewasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (lGP) Camilus Wambura kwa kumpongeza Waziri wa Madini kwa kuzindua kituo hicho.
Wengine aliowashukuru ni wananchi wa kata hiyo na kuwaomba ushirikiano wa kuwa karibu na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kata hiyo kuendelea kuwa salama.
"Jukumu letu kwa sasa ni kuleta askari kwenye kituo hiki, wananchi mnakaribishwa kutoa malalamiko yenu lakini pia nawaomba msiwe mbali na Polisi kwani kazi za Polisi si zetu peke yetu tunawategemea katika kukilinda kituo hiki ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za wahalifu ili ziweze kushughulikia kwa haraka kwa lengo la kutimiza ujengwaji wa kituo hiki" alisema Kamanda Senga.
Naye, Mtendaji Mkuu wa Mgodi huo Ismail Diwani alisema kuwa lengo la kujenga kituo hicho ni kuendeleza ushirikiano na taasisi za Serikali kwa ajili ya kufikisha huduma kwa jamii hasa katika masuala ya elimu, afya na usalama ili jamii iendelee kuwa salama katika maendeleo ya uchumi wa taifa.

Ikumbukwe kuwa Kituo cha Polisi Ngwala kilitarajiwa kuzinduliwa Aprili 28, 2025 ila ilishindikana kutokana na sababu mbalimbali za kazi za kitaifa za Mh. Waziri Mavunde. Kituo hicho kinalenga kuwa muarobaini kwa wakazi wote wa Kata ya Ngwala pamoja na maeneo jirani ya kata hiyo.

No comments