Thursday, June 5, 2025

𝗜𝗟𝗔𝗡𝗜 𝗠𝗣𝗬𝗔 𝗜𝗠𝗘𝗕𝗘𝗕𝗔 𝗠𝗔𝗧𝗨𝗠𝗔𝗜𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗪𝗔𝗧𝗔𝗡𝗭𝗔𝗡𝗜𝗔-𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗠𝗔𝗞𝗔𝗟𝗟𝗔

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi an Mafunzo wa chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, akizungumza na wananchi wa Mto wa Mbu wilayani Monduli mkoani Arusha leo Juni 5,2025.

Na Mwandishi Wetu, Monduli

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2025/2030 waliyoizundua imebeba matumaini kwa watanzanania kwani imebeba mambo muhimu yanayowagusa watanzania.

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi an Mafunzo wa chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla ameeleza hayo leo Juni 5 wakati alipopita kusalimia wananchi katika eneo la Mto wa Mbu wilayani Monduli mkoani Arusha akiwa njiani kuelekea Karatu kwa ajili ya Mkutano wa hadhara akiendelea na ziara yake katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

Amesisitiza ilani hiyo iliyozinduzuliwa imetokana na tathmini ya ilani iliyopita kwa kufanya utafiti na ushirikishwaji wa wananchi, asasi za kiraia na wadau mbalimbali ili kujua vipaumbele na mahitaji ya watanzania.

Makalla amesema ilani hiyo inakwenda kushughulika na ajira, kuimarisha uchumi, miundombinu na changamoto zote zinazowakabilia watanzania na muda utakapofika watainadi kwa sabbau ni ilani ya watanzania kwa sababu inahusu utatuzi wa changamoto zinazowakabili.

“Inaenda kushughulika na maisha ya watanzania kwahiyo ahadi yetu muda utakapofika tutakwenda kuinadi ilani hiyo ni ilani yenu ninyi ndo mustakabari wa maisha ya watanzania kwani hakuna chama chenye Ilani nzuri zaidi ya CCM,” amesema Makalla.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda akizungumza wakati wa mkutano wa wananchi wa Mto wa Mbu wilayani Monduli mkoani Arusha, wakati wa ziara ya Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi an Mafunzo wa chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla leo Juni 5,20

Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fredi Lowassa akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara Mto wa Mbu wakati wa ziara ya Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi an Mafunzo wa chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla

No comments:

Post a Comment