Amri ya Trump kuzuia raia kutoka nchi za kiislamu yapata pigo jingine mahakamani
![]() |
Trump alipiga marufuku baadhi ya raia kutoka nchi za kiislamu kuingia Marekani. (Getty Images) |
Mahakama ya rufaa
nchini Marekani imemua kuwa uamuzi wa kuzuia mpango uliofanyiwa
marekebisho wa marufuku ya Rais Donald Trump kuzuia watu kutoka nchi
sita za kiislamu utasabaki kuwepo.
Rufaa hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya rufaa ya San Fransisco, ni kufuatia umamuzi uliotolewa kupinga raia wengi wao wakiwa kutoka nchi za Kiislam kuingia Marekani.
Hata hivyo mahakama haikusema kuwa serikali inatakiwa kuzipitia upya taratibu za ukaguzi kwa watu wanaoingia nchini humo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Sean Spicer ameutetea msimamo huo wa rais Trump,akisistiza kuwa kila lilalowezekana linatakiwa kufanywa kwaajili ya ulinzi wa Marekani
"Nadhan wote tunafahamu kuwa hizi ni nyakati za hatari dhidi ya tishio la ugaidi,tunapaswa kuwa kulinda kuingia kwa watu wanaoweza kufanya vitendo vya ugaidi na uwagaji wa damu.Tunaendelea kuwa na Imani kwamba amri za rais wetu ni kwa mjibu sheria na kwamba tunaamini mahakama ya juu itazipitisha"
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Washington, Frosh Mwana Maryland's Attorney Generel, Brian Frosh, ameseama Trump kujihusisha biashara akiwa madarakani ni kuvunja katiba
"Aliiteuwa Hoteli yake ya kimataifa ya Trump kwaajili ya wanadiplomasia na maofisa wa serikali. Amekuwa akionekana kwenye sehemu nyingi za biashara zake na imekuwa kama sehemu ya kutangaza biashara hizo.
Analipwa na makampuni yanayo milikiwa na nchi za nje kama vile China ambao pia ni wapangaji katika majengo yake. Na amekuwa akiendelea kuchukua malipo kutoka nchi za Saudi Arabia, India, Afghanistan na Qatar nchi ambazo zina hisa majengo yake ya kibiashara yajulikanayo kama Trump World Tower.
![]() |
No comments