Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza
Polisi katika mji
wa Manchester nchini Uingereza wanasema watu 19 wameuawa na wengine 50
kujeruhiwa kwenye mulipuko uliotokea ndani ya ukumbi wa tamasha la
muziki.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi.
Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misururu ya milipuko mjini London.
![]() |
| Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza. (Haki miliki ya picha Peter Byrne) |
Mashahidi wamesema kuona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya vilipuzi.
![]() |
| Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza. (Haki miliki ya picha Peter Byrne) |
Wakati huo huo Waziri Mkuu Theresa May anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama baadaye leo.
![]() |
| Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza.(Peter Byrne) |
Watu 19 wauwawa kwenye mlipuko Manchester Uingereza








No comments