Mbuzi kushindana Septemba 24
Vijana wakiwa na mbuzi waliokuwa wakiwafundisha wa Ultimate Security kwa ajili ya kushiriki mbio za mbuzi zilizofanyika mwaka jana barabara ya Kenyata Oysterbay jijini Dares Salaam. Foto:fullshangwe
MASHINDANO ya mbio za mbuzi kwa ajili ya kusaidia jamii, yatafanyika Septemba 24, mwaka huu katika Uwanja wa The Green, Dar es Salaam.
Mwandaaji wa mbio hizo, Vanessa Morgan, amesema mashindano hayo ya hisani ya 11, yana lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia asasi mbalimbali za jamii nchini.
Katika uchangishaji huo, wamiliki mbalimbali wa mbuzi, watatoa mbuzi wao waliowapa mafunzo kwa ajili ya kuchuana siku hiyo, ambapo watagawanywa na kuwa makundi saba yatakayoshindana.
Amesema mpaka sasa wametenga sh. milioni 88, kwa ajili ya miradi 14 ya kijamii, ambayo maombi yake yaliwasilishwa kwa wahusika ambapo itachunguzwa na wakurugenzi, Paul Joyson na Abdu Simba na kuifanyia kazi.
Venessa amesema fedha zote zitakazopatikana katika mashindano hayo, zitapelekwa kusaidia asasi ndogondogo ambazo zitatumia msaada huo kwa maendeleo ya kazi zao na kwa faida ya jamii.
Amesema siku hiyo mashabiki wanaweza kushinda vitu mbalimbali, pamoja na kutabiri mbuzi atakayeshinda katika mashindano hayo kupitia katika banda la utabiri lililotolewa na New Africa Casino.
Vanessa alisema watoto wataingia bure ambapo watavikuta vitu vingi vya kuchezea michezo mbalimbali ikiwemo mashindano ya nguo na kofia za kuchekesha.
Mashindano hayo yamedhaminiwa na NBC, British Airways, Coca-Cola, Vodacom, Oryx, Southern Sun na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro.

No comments